Kurasa

Jumanne, 28 Januari 2014

FREEMASON WALITIKISA KANISA LA MZEE WA UPAKO.......

                                           
Ule uvumi kwamba baadhi ya wachungaji,maaskofu na mitume wa makanisa ya kiroho nchini wanajihusisha na imani za Freemasoni unazidi kushika kasi huku awamu hii rungu likimuangukia Mchungaji Anthony Lusekelo almaarufu Mzee wa Upako wa kanisa la GRC ubungo na kutikisa kanisa,,,gazeti la UWAZI linanyetisha.
                                           
                                           MCHUNGAJI ANTHONY LUSEKELO
Madai hayo ya mtumishi huyo kujihusisha na imani hiyo yalianza kuenea kwa kasi mithili ya moto nyikani huku baadhi ya watu wakionyesha shaka juu ya uponyaji wa mtumishi huyo kufuatia miujiza ya ajabu ambayo amekuwa akionyesha kwa watu wenye uhitaji wa kiimani.
                                              MATENDO YA SHAKA
Baadhi ya matendo ambayo yamekuwa yakiwatia shaka baadhi ya watu ni pamoja kitendo cha  mchungaji
huyo kuwaombea watu wakiwa hawana kitu kabisa lakini baada ya muda hurudi kanisani hapo wakiwa na magari ya kifahari na wakionyesha kila dalili ya ukwasi{utajiri}
"ETI UNAKUTA MTU HANA KITU AMEKWENDA KUOMBEWA BAADA YA MIEZI MICHACHE ANARUDI NA GARI LA KIFAHARI KWELI????hayo ni maneno ya ya baadhi ya waumini wa makanisa ya kikristo walipozungumza na UWAZI.
                                               
                                         
                                       ALAMA NA VIASHIRIA TATA.
Wakiafafanua kwa kina juuya wasiwasi wao na mzee wa Upako na miujiza yake,waumini hao walitolea mfano baadhi ya viashiria kuwa ni moja ya utambulisho wa Freemasoni.
Wanasema "mara nyingi mtumishi huyo akiwa madhabahuni amekuwa akitumia kitambaa kikubwa kujifutia na kuwagusia watu anaowaombea hali ambayo huwafanya kuanguka ovyo na kupga kelele ovyo"walisema.
Mbali na kitambaa walisema mtumishi huyo amekuwa akionekana na pete zenye picha za ajabu akiwa anahubiri na kutenda niujiza.
Hofu yao nyingne ni kwamba mtumishi huyo amekuwa hataji neno Mbinguni badala yake husema"MUNGU WANGU AWABARIKI"
                     KAMA KAWAIDA UWAZI HAWABAHATISHAGI WAKAMUIBUKIA OFISINI...
Viranja wa gazeti la uwazi wakamuibukia ofisini kwake Ubungo Kibangu na kumkuta kajaa tele wakamsomea mashtaka bila kumumunya maneno.....
Naye akajibu bila kupepesa macho.......
"Hizo tuhuma zilianza kusikika zamani sana,watu walianza kunituhumu kwenye matumizi ya bendera ya Taifa kanisani,nikaacha wakahamia kwenye kitambaa"
           ANAZIDI KUFUNGUKA ........
"Jamani natumia muda mwingi kusimama madhabahuni sasa nikitumia kitambaa cha 500 itwezekana kweli?????natumia kitambaa kidogo kufuta jasho ishakuwa nongwa."
         UYU APA TENA LUSEKELO.....
"Baadaye wakahamia pete.....mimi ni mtu smart{msafi}na nimezaliwa mjini{borntown}sasa kuvaa pete ni sehemu ya maisha ya mjini lakini baada ya maneno nikavua na sasa sina ...alisema..
         KUHUSU FREEMASON.......
"Sijawahi hata siku moja kuwa Freemason kwanza hata wanapopatikana sipajui,mimi si muumini wa dini wala imani yeyote ya kishetani.......!!!!!SHETANI MWENYEWE ANANIOGOPA........
HII NDIO BONGO TUNAKUTIA MOYO MTUMISHI KUMBUKA MAJARIBU NI SEHEMU YA HUDUMA YAKO NA VIKWAZO HAVINA BUDI KUJA..........!!!!!!!



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni