Judith Wambura,mwanamuziki wanyimbo za kizazi kipya amekana taarifa ya kwamba anatoa mikopo kwa wajasiliamali kupitia ac yake ya facebook.
Kupitia meneja wake,Gardner G Habash,jaydee amesema kwamba ac inayotumika kutapelia watu ni ile ya JUDITH WAMBURA JIDEE MACHOZI ambayo ni feki...{amesema binti machozi akizungumza na
HNB}.Na hapa anasema"Watu wanazidi kuibiwa na wananilalamikia mimi,ngugu zangu wapendwa kuweni makini sana,mimi sina akaunti yeyote inayotoa mikopo Facebook".
Na pia akatoa ushauri na hapa anasema"Nawashauri kama mnataka mikopo mkafungue ac bank ndio huwa wanatoa mikopo na sio mimi,watu wezi wanatumia majina ya watu kujipatia fedha kwa ulaghai".
Mwimbaji huyo aliyeachia wimbo wake mpya 2014"HISTORIA"alisema ashatoa taarifa zaidi ya mara tatu lakini watu bado wanaendelea kuhadaika na wezi hao,Akasema'mimi mwenyewe nataka mkopo hapa nilipo ,halafu nitangaze kutoa?nasikia ukurasa wa Jide feki umetoa mpaka tangazo kwenye TV,,,,JAMANI MIMI SITOI MIKOPO NATOA NYIMBO NA VIDEO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni