Kurasa

Jumapili, 26 Januari 2014

BASATA YAFUNGIA NIMEVURUGWA YA SNURA.....isome hapa.......

BARAZA la Sanaa la Taifa [Basata]limeifungia videpo ya wimbo wa NIMEVURUGWA ya  mwanadada mkali wa mduara Snura Mushi kwa madai ya kukosa maadili kwa jamii.
   Akizungumza hivi karibuni,Snura alisema hajui  sababu gani iliyofanya kazi yake kufungiwakupigwa katika vituo vya telivisheni.

 "Nilipigiwa simu na rafiki zangu na kuambiwa hivyo,lakini mpaka sasa sijui ni kwa sababu gani kwa maana sioni kama nimefanya kitu cha ajabu katika video hiyo na cha kushangazwa hata sijaulizwa na yeyote,ila ndio hivyo"alisema mamaa Majanga.
Snura anasema wakati anasambaza wimbo wa"Majanga"kuna baadhi ya mashabiki wake walimshangaa kwa nini hajachezaamesababisha video ya wimbo huo kupooza na kutokuwa na mvuto ikabidi nisiwaboe mashabiki wangu ndio wimbo uliofuata ikanibidi kucheza kumbe nilikuwa naandaa mazingira ya kufungiwa.alisema Snura.
  Snura ni kati ya wasanii ambao wanafanya vizuri katika vituo mabimbali vya redio na televisheni kutokana na kazi zake ambazo zinaliteka soko la muziki nchini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni