Kurasa

Ijumaa, 7 Februari 2014

NI LULU TENAAAA.......NI FEBRUARI 17 KESI YAKE KURINDIMA TENA...........isome hapa

KESI ya mauaji bila kukusudia inayomkabili msanii wa filamu nchini Bi. Elizabeth Michael{LULU}inatarajia kuunguruma katika mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam,februari 17 mwaka huu. Kesi hiyo ambayo ilibadilika kutoka kwenye kesi ya mauaji ya kukusudia na kuwa mauaji ya bila kukusudia ilipangwa kusikilizwa mbele ya jaji Rose Teemba... Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya mahakama hiyo mshitakiwa huyo anayetetewa na wakili Peter Kibatala atasomewa mashtaka yanayomkabili upya na atatakiwa kujibu kama ni kweli aliua bila kukusudia au hapana.... Lulu baada ya kubadilishiwa mashitaka na kushitakiwa kwa kuua bila kukusudia alipata dhamana na kupewa masharti ya kuripoti kwa msajili wa mahakama hiyo kila mwezi. Awali mwaka 2012,mshitakiwa alipandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa madai ya kumuua msanii nyota wa filamu nchini,Steveni Kanumba. Inadaiwa kuwa,Lulu na Kanumba wablikuwa na walikuwa na mahusiano ya kimapenzi na waligombana usiku wa April 6,2012 na April 7 mwaka huo katika eneo la Sinza Vatican Kanumba aliaga dunia..... KILA LA KHERI LULU

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni