Kurasa

Jumatatu, 14 Aprili 2014

JK AMLILIA MUHIDIN GURUMO,,,KUZIKWA LEO........

Tanzania imepata pigo kwa kumpoteza mwanamuziki mkongwe Muhidin Gurumo{74} aliyefariki dunia juzi katika hosipitali ya Taifa ya Muhimbili,Dar es Salaam.
Mzee Gurumo alifariki dunia kutokana na maradhi ya moyo baada ya kulazwa katika hospitali ya MHN kwa siku tatu. Agosti mwaka jana mzee Gurumo alitangaza rasmi kustaafu muziki baada ya kuitumikia fani hiyo kwa muda wa miaka 53.Alifanya hivyo kutokana na umri na afya yake kuzorota.... Gurumo alizaliwa mwaka 1940,alianza muziki mwaka 1960akiwa na bendi ya Kilimanjaro,,,mwaka 1962 alijiunga na Rufiji Jazz Band kabla ya kutua Kilwa Jazz mwaka 1963. Mwaka 1964,akiwa mwasisi wa NUTA Jazz Band ambayo ilipita hatua nyingi kwa majina ikiwa inaitwa Juwata Jazz,OTTU,MSONDO, na sasa MSONDO JAZZ BAND aliyodum nayo mpaka kustaafu muziki japo alichomoka mwaka 1978 DDC Mlimani Park Sikinde... Kwa upande mwingine Raisi wa Jamhuri ya Muungano Mh.Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Habari,vijana utamaduni na michezo,DK Fenella Mkangarakutokana na kifo cha Gurumo.... "NIMESIKITISHWA NA KUHUZUNISHWA NA TAARIFA YA KIFO CHA MAALIM GURUMO AMBAYE ALIKUWA MMOJA WA WASANII WA DANSI WALIOTUMIKIA TAIFA HILI KWA BIDII TANGU MIAKA YA SITINI KUPITIA SANAA YA MIZUKI KUPITIA BENDI MBALIMBALI ZA DANSI TANGU AKIWA NUTTA JAZZ,MLIMANI PARK,MPAKA MSONDO NGOMA AMBAYO AMEITUMIKIA AHDI ALIPOSTAAFU MWAKA 2013"alisema Rais Kikwete katika salamu zake..... Alisema mchango wa Gurumo katika taifa hili ni mkubwa na wa kuigwa mfano kutokana na kipaji alichojaaliwa na Mwenyezi Mungu ambacho alikitumikia kikamilifu kwa manufaa ya watanzania kwa ujumla... Raisi Kikwete alimtaka Dk.Mkangara kufikisha salamu zake za rambi rambina pole kwa familia ya marehemu Gurumo kwa kumpoteza kiongozi na mhimili wa familia yao.. Mwili wa Marehemu Gurumo utawasili nyumbani kwake Makuburi Ubungo Wilaya ya Kinondoni saa mbili asubuhi,baada ya hapo kutakuwa na taratibu nyingine za mazishi ambapo kutakuwa na risala mbalimbali kutoka kwa ndugu pamoja na chama cha muziki wa Dansui Tanzania{CHAMUDATA} Majira ya saa tano itaanza safari ya kuupeleka mwili kijijini kwao Masaki wilaya ya Kisalawe,Mkoani Pwani kwa mazishi.... MZEE GURUMO WEWE MBELE SISI NYUMA YAKO,,PUMZIKA KWA AMANI GWIJI LA MIZIKI TANZANIA........AMEEEN